Uzinduzi wa kituo hicho uliofanyika tarehe 2,Oktoba, 2026, unatarajiwa kurahisisha upatikanaji wa huduma za kipolisi na kuimarisha hali ya ulinzi na usalama kwa zaidi ya wananchi 18,000 katika eneo hilo, huku ukuaji wa Mji wa Isaka ukiongeza umuhimu wa kuwa na kituo cha polisi chenye uwezo wa kutoa huduma kwa wakati.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo, Kamanda Magomi ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na wananchi katika kufanikisha ujenzi wa
kituo hicho.
Amesema
Jeshi la Polisi litahakikisha kituo hicho kinapatiwa askari wa kutosha, ili
huduma za usalama ziweze kutolewa wakati wote, akieleza kuwa mji wa Isaka
unaendelea kukua kutokana na shughuli za kiuchumi zinazochochewa na uwepo wa
Bandari Kavu.
Aidha, Kamanda Magomi amewataka askari watakaohudumu katika kituo hicho kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni zinazowaongoza katika utendaji kazi.
Kwa upande
wake, Mbunge wa Jimbo la Msalala, Mh. Mabula Magangila, amempongeza Kamanda
Magomi kwa juhudi anazozifanya katika kuimarisha amani na utulivu mkoani
Shinyanga.
Mh.
Magangila amesema, kuimarika kwa Falsafa ya Polisi Jamii kumechangia
kubadilisha mtazamo wa vituo vya Polisi, kutoka kuwa maeneo yanayoonekana zaidi
wakati wa uhalifu na kuwa vituo vya kutoa huduma, malezi na kuzuia uhalifu
kabla haujatokea.
Amesema anatamani utamaduni huo uendelee kuimarika na kutawala katika vituo vyote vya Polisi nchini.
Kituo kipya cha Polisi Isaka kimegharimu zaidi ya Shilingi Milioni 236, mpaka kukamilika kwake, ambapo kati ya hizo, Shilingi Milioni 210 zimetolewa na Serikali kupitia makao makuu ya Polisi na Shilingi Milioni 26 na 855,000/= zinatokana na michango ya wananchi.
Fedha hizo, zimetumika kwa shughuli mbalimbali za ujenzi pamoja na ununuzi wa Samani za ndani na mahitaji mengine yanayotakiwa katika kituo cha Polisi.






0 Comments