
Katenda
amesema wananchi wanapaswa kuondokana na dhana ya kutafuta bima ya afya pale tu
wanapokuwa na mgonjwa anayehitaji matibabu ya muda mrefu, na badala yake
wajenge utamaduni wa kujiunga mapema na bima hiyo ili kuwa na uhakika wa kupata
nafuu ya huduma za afya kwa familia zao.
Amesema NHIF
inaendelea kupokea wanachama wapya wakati Serikali ikiendelea kukamilisha
mchakato wa utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote, huku akibainisha kuwa
mwongozo zaidi utatolewa kwa wale watakaokutwa wamejiunga na NHIF mara baada ya
mchakato huo kukamilika.
Katenda
ameeleza kuwa, NHIF kwa sasa inatoa vifurushi mbalimbali kulingana na mahitaji
ya wananchi ambavyo vimegawanywa katika makundi matano ya Tarangire, Ngorongoro
afya, Mikumi, Serengeti na Tanzanite ambavyo vinaambatana na punguzo kubwa kwa
wale wanaojiunga kifamilia.
Katenda
amesema huduma za NHIF zinapatikana kwenye zaidi vituo zaidi ya 10,000 vya
kutolea huduma za afya nchini, kuanzia ngazi ya zahanati, vituo vya afya, hospitali
za wilaya, Hospitali za rufaa za mikoa na kanda hadi hospitali za taifa.
Amefafanua
kuwa vifurushi vyote vinajumuisha huduma muhimu za vipimo na dawa, huku tofauti
kubwa ikiwa katika wigo wa huduma na mahitaji maalumu ya wanachama.
Pia
amewataka wananchi kujenga tabia ya kutembelea ofisi za NHIF zilizopo karibu yao
ili kupata elimu sahihi kuhusu huduma za bima ya afya, masharti ya kujiunga na
vifurushi vinavyowafaa kulingana na mahitaji yao.
Amesema
hatua hiyo itasaidia kuondoa upotoshaji wa taarifa na kuwawezesha wananchi
kufanya maamuzi sahihi na kwamba bima ya afya si gharama ikilinganishwa na
utaratibu wa kawaida wa matibabu, bali ni uwekezaji muhimu unaowasaidia
kukabiliana na changamoto za kiafya bila kuathiri hali zao za kiuchumi.
Kuhusu utekelezaji
wa Bima ya Afya kwa wote, Katenda amesema kwa sasa huduma hiyo imeanza kutolewa
kwa kaya zisizo na uwezo zinazotambuliwa kupitia Mpango wa TASAF, ambapo
Serikali inagharamia huduma hiyo kwa asilimia 100.
Ameongeza
kuwa makundi mengine ya wananchi yataanza kunufaika na Bima ya afya kwa wote
mara tu mchakato utakapokamilika.
0 Comments