PAPA LEO XIV ATIMIZA MIAKA 71 YA KUZALIWA

 

Baba Mtakatifu Papa Leo XIV,  leo Septemba 14, 2026, ametimiza miaka 71 ya kuzaliwa, ikiwa ni siku ambayo Kanisa Katoliki linaadhimisha Sherehe ya Kutukuka kwa Msalaba.

Katika maadhimisho hayo, Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Italia (CEI) limetuma salaam kwa Papa Leo XIV, likimtakia heri ya siku yake ya kuzaliwa na kumshukuru kwa huduma yake kwa Kanisa na kwa mikutano mbalimbali aliyofanya na Kanisa la Italia katika kipindi cha miezi iliyopita.

CEI imesema mafundisho ya Papa Leo XIV yameendelea kusisitiza umuhimu wa maisha ya Kanisa yanayojengwa katika imani, kukutana na Kristo aliyekufa na kufufuka, pamoja na jumuiya zinazoshiriki katika utangazaji wa Injili, utume na huduma.

Aidha, Baraza hilo limeeleza kuwa linazingatia kwa namna ya pekee ujumbe wa Papa kuhusu uhusiano kati ya msamaha na amani, hasa katika kipindi ambacho vita na migogoro vinaendelea kuikumba sehemu mbalimbali duniani.

CEI imemhakikishia Papa Leo XIV kuwa, Kanisa la Italia litaendelea kuwa karibu na watu wanaoteseka kupitia matendo ya mshikamano.

Papa Leo XIV, alizaliwa Septemba 14, 1955, huko Chicago, Illinois, nchini Marekani, ambapo alipewa na wazazi wake jina la Robert Francis Prevost.

Alichaguliwa kuwa Papa mnamo Mei 8, 2025, kufuatia kifo cha Papa Fransisko kilichotokea Aprili 21, 2025.

Ni Papa wa kwanza kutoka Marekani na Amerika Kaskazini, na ni mtawa wa Shirika la Mtakatifu Augustino (OSA).

 

Post a Comment

0 Comments