Akizungumza
na SHINYANGA ONE MEDIA, Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi
Hadija Mborouk, amesema kukatika kwa umeme kumetokana na hitilafu iliyotokea
katika kituo cha kupozea umeme cha Matanda, kilichopo mjini Shinyanga, na kuathiri sehemu kubwa ya mji wa Shinyanga.
Mhandisi
Mborouk amesema mafundi wa TANESCO wanaendelea na kazi ya kubaini na kurekebisha
hitilafu hiyo, ambapo makao makuu ya Kanda ya Magharibi (Tabora) wametuma
wataalam kuja kuongeza nguvu katika zoezi la kurejesha huduma hiyo.
Amewaomba wananchi kuwa na subira wakati TANESCO ikiendelea na jitihada za kutatua tatizo hilo na kurejesha huduma ya umeme katika maeneo yaliyoathirika.

0 Comments