Meneja wa
TANESCO mkoa wa Shinyanga Mhandisi Hadija Mborouk, ameiambia SHINYANGA ONE
MEDIA kuwa, mafundi wamefanya kila
linalowezekana kuhakikisha huduma za umeme zinarejea, ambapo kupitia jitihada walizozifanya umeme umerudi majira ya saa kumi na mbili
jioni.
Mhandisi
Mbarouk amewashukuru wananchi kwa ushirikiano na uvumilivu walioonyesha
katika kipindi chote cha matengenezo.
Amewaomba kutoa taarifa TANESCO endapo kutakuwa na eneo lolote ambalo halijapata huduma ya umeme na kwamba, mafundi wako tayari muda wowote kutoa huduma.

0 Comments