Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali
Kauli hiyo
imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Florent Laurent Kyombo, Jumamosi tarehe 17, Oktoba, 2026, baada ya Kamati
kutembelea na kukagua ujenzi wa wodi ya kisasa ya Mama na Mtoto katika
Hospitali ya Manispaa ya Kahama, Kituo Kikuu cha Mabasi Mbulu kinachoendelea
kujengwa katika Kata ya Nyasubi, Soko la Sango linaloendelea kujengwa katika
Kata ya Nyasubi, Kituo Kidogo cha Mabasi
Zongomela na Soko la Wajasiriamali Wadogo Zongomela ambavyo vyote vinajengwa
katika Kata ya Zongomela.
| Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya TAMISEMI Florent Laurent Kyombo |
| Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kahama Mataluma Kaniki |
Kyombo
amewataka viongozi wa Mkoa wa Shinyanga na Wilaya ya Kahama kusimamia miradi
hiyo kwa karibu ili ikamilike kwa wakati, huku akisisitiza kuwa, wananchi waliokuwa
wakifanya shughuli za kibiashara katika maeneo ya miradi ya masoko na vituo vya
mabasi wapewe kipaumbele katika ugawaji wa vibanda.
Aidha, ameshauri gharama za upangishaji wa vibanda zizingatie uwezo wa kiuchumi wa wananchi, pamoja na kutengwa kwa maeneo ya kutolea huduma muhimu ikiwemo vituo vya polisi kwa ajili ya usalama na huduma ya kwanza kwa watu wanaopata changamoto ya kiafya.
| Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama Masudi Kibetu |
| Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, John akizungumza mbele ya Kamati ya TAMISEMI |
| Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Pili Mnyami akizungumza mbele ya Kamati ya TAMISEMI |
Naye Mbunge
wa Jimbo la Kahama, Benjamin Ngaiwa, ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita
chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka fedha nyingi kwa ajili ya
kutekeleza miradi mbalimbali katika Jimbo lake, huku akiwahimiza wananchi
kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuwaletea maendeleo.
Pia, amemtaka mkandarasi kuhakikisha vituo vya mabasi vinatengewa maeneo maalumu kwa ajili ya maegesho ya bajaji na pikipiki, ili kuwawezesha vijana waliojiajiri kupitia biashara hiyo kunufaika na uwepo wa miradi hiyo.
| Mbunge wa Jimbo la Kahama, Benjamin Ngaiwa |
Akizungumza
kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Peter
Masindi, amemshukuru Rais Dkt. Samia kwa ufadhili wa miradi hiyo mikubwa ya
Kimkakati na kuwahimiza wananchi wa Kahama kutumia fursa za kiuchumi
zitakazotokana na miradi hiyo kufanya kazi kwa bidii na kuwekeza kwenye biashara,
kwa kuwa tayari Serikali imewawekea mazingira wezeshi ya kujikwamua kiuchumi.
Pia, amewashauri wajasiriamali wadogo kuchangamkia mikopo yenye masharti nafuu inayotolewa na Serikali kupitia Benki ya NMB, ili kuongeza mitaji yao.
| Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Peter Masindi akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama mbele ya Kamati ya TAMISEMI na wananchi |
| Mhandisi Mshauri wa Manispaa ya Kahama Samuel Mtawa akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi mbele ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya TAMISEMI |
Kwa upande
wa miradi ya Kituo Kikuu cha Mabasi Mbulu, Soko la Sango, Kituo Kidogo cha
Mabasi Zongomela na Soko la Wajasiriamali Wadogo Zongomela ambayo ilianza kutekelezwa
Desemba 31, 2024, inatarajiwa kukamilika Desemba 30, 2026.
0 Comments