Kamanda Magomi ametoa wito huo wakati akitoa elimu kwa wananchi wa Kata za Wendele na Kagongwa katika Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, kupitia kampeni maalumu ya Ongea na Kamanda wa Mkoa wa Shinyanga, inayolenga kusikiliza na kutatua kero za kiusalama kwa wananchi kwa njia ya mazungumzo ya ana kwa ana.
Amesema
baadhi ya wanaume wanaofanyiwa ukatili ndani ya familia wamekuwa wakishindwa
kutoa taarifa kwa sababu ya aibu na hofu, hali inayochangia kuendelea kwa vitendo
hivyo.
Amewasisitiza
kutambua kuwa, sheria inawalinda wanawake na wanaume bila ubaguzi, hivyo
hawapaswi kuogopa kuripoti matukio hayo.
Pamoja na
kuwepo kwa wanaume wanaofanyiwa ukatili na wanawake, baadhi yao wameendelea
kuvumilia hali hiyo kimya kimya, tofauti na wanawake ambao wamekuwa
wakijitokeza kutoa taarifa wanapofanyiwa vitendo vya ukatili.
Katika hatua
nyingine, Kamanda Magomi amesikiliza na kushughulikia kero mbalimbali za
wananchi, ambapo suala la utoaji wa dhamana kwa watuhumiwa wa makosa
yanayodhaminika limeendelea kuibuliwa.
Akizungumzia suala hilo, Kamanda Magomi amesisitiza kuwa, dhamana kwa makosa yanayodhaminika hutolewa bila malipo katika vituo vya polisi. Amewataka wananchi kutoa taarifa kwa viongozi wa juu wa Jeshi la Polisi endapo watabaini askari anayedai fedha kwa ajili ya kutoa dhamana kwa ndugu zao.
Wakati
huohuo, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kahama, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP)
Maro Kenyunko, ametoa makoti 10 ya mvua kwa kikundi cha Sungusungu katika
Kata ya Wendele, ili kuwasaidia kujikinga na mvua wanapotekeleza majukumu ya
doria kupitia ulinzi shirikishi.
Hatua hiyo
imefuatia ombi lililowasilishwa na Sungusungu kwa Jeshi la Polisi la kuhitaji
makoti hayo kwa ajili ya kurahisisha utekelezaji wa majukumu yao ya ulinzi na
usalama.
Kupitia kampeni hiyo, Kamanda Magomi amewahimiza wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yao, kulinda amani na kusalimisha kwa hiari silaha haramu walizonazo.



0 Comments