MAZISHI YA BABA MZAZI WA MKURUGENZI MTENDAJI WA RAFIKI-SDO KUFANYIKA OKTOBA 16


Marehemu Mzee Samwel Ng’ong’a Owuor


Mazishi ya marehemu Mzee Samwel Ng’ong’a Owuor, Baba mzazi wa
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kutetea Haki za Vijana, Wanawake na Watoto (RAFIKI-SDO), Bw. Gerald Ng’ong’a, yanatarajiwa kufanyika Ijumaa, Oktoba 16, 2026, katika Wilaya ya Rorya, mkoani Mara.

Shughuli za kuomboleza msiba huo zinaendelea nyumbani kwa Bw. Gerald Ng’ong’a ambaye ni mtoto wa Marehemu,  Kizumbi katika Manispaa ya Shinyanga, karibu na Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Kizumbi.

Kwa mujibu wa Bw. Gerald ambaye pia ni Mwenyekiti Mstaafu wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, shughuli za mazishi ya Baba yake zitatanguliwa na Ibada maalum ya kuaga na kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu, itakayofanyika kuanzia saa 6:00 mchana, siku ya Jumatano, Oktoba 14, 2026, huko Kizumbi katika Manispaa ya Shinyanga.

Mkurugenzi Mtendaji wa RAFIKI-SDO na Mwenyekiti Mstaafu wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya Bw. Gerald Ng’ong’a

Ibada hiyo pia itaambatana na kupokea salamu za rambirambi kutoka kwa makundi mbalimbali, ndugu, jamaa na marafiki.

Mwili wa marehemu utasafirishwa alfajiri ya Alhamisi, Oktoba 15, 2026, kuelekea Rorya kwa ajili ya mazishi, yatakayofanyika siku inayofuata ya Ijumaa tarehe 16, Oktoba 2026.

Mzee Samwel Ng’ong’a Owuor, amefariki dunia Oktoba 2, 2026, akiwa na umri wa miaka 96, wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Kolandoto, iliyopo Manispaa ya Shinyanga.

Mungu ailaze roho ya marehemu Mzee Samwel Ng’ong’a Owuor mahali pema peponi. Amina.

Post a Comment

1 Comments

  1. Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi,Amin

    ReplyDelete