MADEREVA SITA SHINYANGA WAFUNGIWA LESENI ZA UDEREVA

 

Jumla ya madereva 6  wa magari, wamefungiwa leseni  zao za udereva, baada ya kubainika kutenda makosa yanayokiuka sheria za usalama barabarani.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi, madereva hao  walibainika kutenda kosa la kuendesha magari kwa mwendokasi wa Kilomita 116 kwa saa, kwenye maeneo yasiyoruhusiwa, kinyume na sheria za usalama barabarani.

Kamanda Magomi amebainisha kuwa, hatua hiyo imechukuliwa kupitia operesheni iliyofanyika katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia Juni hadi Agosti, 2026, iliyofanyika kwa lengo la kudhibiti vitendo vya uhalifu, ikiwemo kuimarisha usalama barabarani.

Kupitia Operesheni hiyo, kikosi cha usalama barabarani kilibaini jumla ya makosa 5, 291, ya ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani, ambapo kati ya hayo, makossa 4,079, yalihusisha magari na 1, 212, yalihusisha bajaji na pikipiki.

Kamanda Magomi amebainisha kuwa, wahusika wote walichukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria, ikiwemo kulipa faini za papo kwa papo.

Kufuatia hali hiyo, Kamanda huyo wa Polisi amewataka madereva na watumiaji wengine wa barabara kuzingatia sheria za usalama barabarani, ili kuepusha ajali zinazogharimu maisha ya watu, kusababisha ulemavu wa kudumu pamoja na uharibifu wa mali.

 

Post a Comment

0 Comments