NCHIMBI AFUKUZWA UANACHAMA WA CCM, NDEJEMBI KURITHI UMAKAMU WA RAIS

Aliyekuwa Makamu wa rais na Katibu Mkuu wa zamani wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi amefukuzwa uanachama wa chama hicho.

Dk Nchimbi amefukuzwa unachama siku moja baada ya kumwandikia barua Rais Samia Suluhu Hassan kumwomba kujiuzulu nafasi ya Makamu wa Rais ambapo ombi hilo lilikubaliwa.

Uamuzi wa kufukuzwa uanachama kwa Nchimbi, umetangazwa usiku wa leo Jumatano, Agosti 26, 2026 na Katibu Mkuu wa CCM, Dk Asha Rose- Migiro, alipozungumza na waandishi wa habari katika ofisi ndogo za chama hicho, Lumumba jijini Dar es Salaam, wakati akitoa taarifa ya maazimio ya vikao vya kamati kuu na Halmashauri Kuu vilivyokutana jijini Dar es Salaam kuanzia asubuhi hadi usiku wa leo Jumatano.

Dk Migiro amesema kulikuwa na ajenda ambazo zilijadiliwa na miongoni ni suala la maadili lililokuwa linamkabili mwanachama huyo wa zamani wa CCM.

Wakati huohuo,Halmashauri Kuu ya CCM imepitisha jina la Deogratius Ndejembi kuwa mrithi wa Nchimbi katika nafasi ya makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya Dkt. Nchimbi kutangaza kujiuzulu nafasi hiyo.

Uamuzi huo unafungua ukurasa mpya katika uongozi wa Serikali na Chama Cha Mapinduzi, huku Ndejembi akitarajiwa kuchukua majukumu yaliyoachwa na Dkt. Nchimbi.

Mabadiliko hayo yamekuja katika kipindi ambacho CCM inaendelea kufanya maamuzi kuhusu muundo na uongozi wa chama pamoja na Serikali.

 


Post a Comment

0 Comments