Meneja wa Kampuni hiyo, Bw. Abita Iman, ameiambia SHINYANGA
ONE kuwa, kampuni imejipanga kwa kuandaa magari maalum ya kuwachukua abiria
kutoka Stendi Kuu ya Magufuli na kuwapeleka hadi katika ofisi zake zilizopo
Manzese Argentina.
Amesema utaratibu huo umelenga kurahisisha usafiri kwa abiria wanaohitaji kwenda maeneo mbalimbali, ikiwemo katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
Meneja wa Kampuni ya Ally's Star, Bw. Abita Iman
Aidha, amesema kampuni imeweka utaratibu wa kuwachukua na
kuwapeleka hadi Stendi Kuu ya Magufuli abiria wanaokata tiketi kupitia ofisi za
Ally’s Star zilizopo Manzese Argentina, ili kuwaondolea usumbufu wa kutafuta
usafiri mwingine.

Ofisi za kampuni ya Ally's Star zilizopo Manzese Argentina Jijini Dar es salaam

Kwa upande wa abiria wanaosafiri kwenda Mwanza na kushukia Stendi
ya Nyegezi, Iman amesema kampuni imeandaa usafiri maalum wa kuwafikisha
katikati ya Jiji la Mwanza, kupitia ofisi zake zilizopo eneo la Nata.
Iman amewaomba wananchi, wakiwemo wakazi wa Shinyanga,
kuendelea kuiamini kampuni hiyo, akisema inatoa huduma kwa kuzingatia mahitaji
ya wateja pamoja na kuweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha hawapati usumbufu
kutokana na mabadiliko ya utaratibu wa usafiri.
Ally’s Star, inayomilikiwa na wawekezaji wazawa kutoka mkoani Shinyanga, hutoa huduma za usafirishaji wa abiria kwa safari za masafa marefu na mafupi katika maeneo mbalimbali nchini.
Safari za kampuni hiyo zinahusisha mikoa mbalimbali, ikiwemo Dar es Salaam, Dodoma, Shinyanga, Mwanza, Mara, Simiyu, Usinge Tabora, Iringa, Mbeya, Katavi na Rukwa.
Bw. Abita Iman akiwa Ofisini kwake
1 Comments
Mnastahiri tuzo pongezi kwenu
ReplyDelete