MUME WA RAIS SAMIA AFARIKI DUNIA

Mume wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Hafidh Ameir, amefariki dunia.
Taarifa za kifo cha Hafidh Ameir (anayeonekana kwenye picha hapo juu akiwa na Mheshimiwa rais) zimetangazwa leo Jumatatu tarehe 07, Septemba 2026, na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, kupitia vyombo vya habari.
Kwa mujibu wa Makamu wa rais, kifo cha Mzee Hafidh kimetokea leo majira ya saa 2 asubuhi wakati akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa moyo katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena, huko Zanzibar.
Mazishi ya Hafidh Ameir yanafanyika jioni ya leo huko Kizimkazi Zanzibar.

Post a Comment

0 Comments