ASKOFU NZELU MGENI RASMI KATIKA JUBILEE YA MIAKA 50 YA SHULE YA SEKONDARI MWADUI

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Dkt. Yohana Ernest Nzelu

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Yohana Ernest Nzelu, k
esho Jumamosi tarehe 10, Oktoba 2026, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya  Jubilee ya miaka 50, tangu kuanzishwa kwa Shule ya Sekondari Mwadui, iliyoko katika Mgodi wa Almasi wa Williamson wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Shule hiyo Mwalimu Mashiku Mashallah, shereha za Jubilee zitaanza saa mbili asubuhi, na zitaambatana na mahafali ya 48 ya wanafunzi wa kidato cha nne.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Mwadui Mwalimu Mashiku Mashallah

Shule ya Sekondari Mwadui ilianzishwa na mgodi wa Williamson mnamo mwaka 1976, ambapo mwaka 1996, mgodi uliikabidhi chini ya  Kanisa la KKKT, ili mgodi huo upate nafasi ya kujikita zaidi na shughuli za uchimbaji.

Kanisa la KKKT limekuwa likiindesha shule hiyo tangu mwaka 1996, ambapo imekuwa ni fursa muhimu ya kielimu kwa watoto wa wafanyakzi wa mgodi huo na kutoka nje ya mgodi.

Kutokana na maendeleo mazuri ya kitaaluma, shule hiyo imekuwa ikipokea wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali nchini, ambao wanakuja kupata elimu ya Sekondari.

Miongoni mwa viongozi waliosoma katika Shule hiyo ni pamoja na Balozi Mstaafu wa Tanzania nchini Brazil, Dkt. John Stephen Simbachawene,  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya rais, Ikulu Bakari Machumu na Mhandisi Mkuu wa Mgodi wa Williamson Shagembe Mipawa.

Post a Comment

0 Comments