| Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Dkt. Francis Mlacha |
Mkutano huo
ambao ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja, umefanyika leo,
Oktoba 8, 2026, katika ukumbi wa The Planet Hotel, Manispaa ya Kahama, na
kufunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Dkt. Francis Mlacha.
Akifungua
mkutano huo, Dkt. Mlacha amesema nishati ya umeme ni moja ya nyenzo muhimu
iliyochangia kwa kiasi kikubwa mabadiliko katika maisha ya watu na maendeleo ya
shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii.
Ameipongeza TANESCO Mkoa wa Shinyanga kwa juhudi inazofanya katika kuwahudumia wananchi na kuitaka kuendelea kuboresha huduma kwa wawekezaji na wafanyabiashara wanaotegemea nishati ya umeme katika kuendesha shughuli zao.
Dkt. Mlacha
amewataka wafanyabiashara na wawekezaji kuendelea kushirikiana na Serikali
katika kuchochea maendeleo ya Mkoa wa Shinyanga, akieleza kuwa uwekezaji unatoa
fursa za ajira kwa wananchi na kuchangia pato la taifa kupitia ulipaji wa kodi.
Aidha,
amesema Serikali haitakuwa tayari kuona wafanyabiashara au wawekezaji
wakinyanyaswa na maafisa wa umma, akisisitiza umuhimu wa kuwepo kwa mazingira
rafiki ambayo yatawezesha kufanya shughuli zao kwa ufanisi na kuchangia
maendeleo.
Kwa upande wake, Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Hadija Mbarouk, amesema shirika limejipanga kuhakikisha linakuwa na vyanzo mbalimbali vya uzalishaji wa umeme kupitia miradi midogo na mikubwa ya kimkakati, ambapo mkoa wa Shinyanga unachangia kupitia Mradi wa Umeme wa Jua ulioko Wilayani Kishapu, unaotarajiwa kuzalisha megawati 150.
| Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Hadija Mbarouk |
Mhandisi
Mbarouk amebainisha kuwa, kwa sasa TANESCO inaendelea kuboresha miundombinu ya
umeme, hatua inayolenga kupunguza changamoto zinazojitokeza na kusababisha
kukatika kwa umeme.
Naye Bi. Sara Libogoma, Afisa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano na Huduma kwa Wateja, Kitengo cha Wateja Wakubwa, Makao Makuu ya TANESCO, amesema shirika linatambua mchango wa wateja wakubwa, ambao amesema, wanachangia takribani asilimia 50 ya mapato ya shirika hilo.
| Afisa kutoka Kitengo cha Wateja Wakubwa, Makao Makuu ya TANESCO Bi. Sara Libogoma |
Amesema
kutokana na mchango huo, TANESCO imeweka kitengo maalum kwa ajili ya
kuwahudumia wateja wakubwa na kushughulikia mahitaji yao kwa ufanisi.
Kwa upande wao, washiriki wa mkutano huo ambao miongoni mwao ni wawekezaji katika Sekta za viwanda na madini, wameishauri TANESCO kuendelea kuboresha huduma zake, ikiwemo kurekebisha changamoto zinazojitokeza katika miundombinu ya umeme ili kupunguza tatizo la kukatika kwa umeme.
Katika
mkutano huo, washiriki pia wamepatiwa elimu kuhusu mifumo mbalimbali
inayotumiwa na TANESCO katika kuwahudumia wateja wakubwa, ikiwemo mifumo ya
Automatic Meter Reading (AMR) na Large Power Users (LPU).
Katika
kuhitimisha mkutano huo, TANESCO imetoa tuzo kwa wateja watatu wanaochangia
kiwango kikubwa cha mapato kwa shirika.
Wateja hao
ni Kampuni ya Jambo Food Products ya Shinyanga, Mgodi wa Almasi wa Williamson
uliopo Mwadui Wilayani Kishapu na Mgodi
wa Dhahabu wa Barrick Bulyanhulu uliopo Msalala, Wilayani Kahama.
Aidha, kampuni nane zimetunukiwa zawadi kwa kulipa bili za umeme kwa wakati, huku wateja wengine 125 wakipewa vyeti maalum vya kutambua mchango wao.
| Mhandisi Mkuu wa TANESCO mkoa wa Shinyanga Benson Mbigili Nasania |
| Meneja wa TANESO wilaya ya Kahama Mhandisi Peter Magari |
| Mhasibu wa TANESCO mkoa wa Shinyanga Rebeka Kajigile |
0 Comments