Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, amewahimiza wakristo kuwa alama ya upendo na mshikamano, wakiongozwa na huruma ya Mungu.
Askofu Sangu
ametoa rai hiyo kwa wakristo, wakati akiadhimisha Misa takatifu ya kulitegemeza
Jimbo, iliyowakutanisha, Mapadre, watawa na waamini kutoka maeneo mbalimbali ya
Jimbo.
Askofu Sangu amewataka wakristo kuongozwa na humuruma ya Mungu, ambayo itawawezesha kuwa kielelezo cha upendo, umoja na mshikamano.
Amewasihi wakristo
kuwa na moyo unaojali shida na mahangaiko ya wengine wanayoyapata katika hali
ya kimwili na kiroho, pamoja na kuwatendea wema.
Wakati
huohuo, Askofu Sangu amewashukuru waamini wa Jimbo la Shinyanga kwa namna
ambavyo wameendelea kujitoa kulitegemeza Jimbo lao, ambapo hatua hiyo ameitaja
kuwa inaliwezesha Kanisa la Shinyanga kujitegemea na kustawi.
Zaidi ya
Shilingi Milioni 240, zimekusanywa kupitia
mpango huo wa kulitegemeza Jimbo, ambazo zimechangwa na waamini kutoka Parokia
24 za Jimbo na Parokia teule 3 za Mwakitolyo, Lyamidati na Masanwa.

0 Comments