PADRE SALAWA AMSHUKURU MUNGU KWA KUTIMIZA MIAKA 31 YA UPADRE

Padre Anatoly Salawa (katikati) akiwa katika adhimisho la Misa ya kumshukuru Mungu kwa kutimiza maiaka 31 ya Upadre

Paroko wa Parokia ya Busanda katika Jimbo Katoliki Shinyanga Padre Anatoly Salawa, tarehe 20, Novemba, 2026, ameadhimisha Misa takatifu ya kumshukuru Mungu, kwa kutimiza miaka 31 tangu apewe daraja takatifu ya Upadre.

Misa imeadhimishwa katika Kigango cha Mtakatifu Yohane Paul II, Tinde Parokia ya Busanda , ambayo imehudhuriwa na Mapadre, watawa na waamini kutoka maeneo mbalimbali.

Katika mahubiri yaliyotolewa naye Padre DonBosco Ngua kutoka Jimbo la Singida, amemwelezea Padre  Salawa kuwa ni miongozi mwa watu waliojitolea maisha yao bila kujibakiza, kwa ajili ya Mungu na Kanisa, huku akifanya utume wake kwa kuongozwa na maisha ya sala na  fadhila ya unyenyekevu.

Padre DonBosco Ngua

Amewataka waamini wakatoliki kuiga mfano wa Padre Salawa wa kutoyumba kiimani hata pale wanapokutana na changamoto mbalimbali za kimaisha.

Aidha, amewaasa wakristo kutokuwa wabinafsi  wala kutumia nafasi zao kuwakandamiza wengine, na badala yake wawe mfano na kielelezo cha wema.

Kwa Upande wake Mbunge wa Jimbo la Itwangi Mheshimiwa Azah Hilal Hamad, ambaye alihudhuria Misa hiyo, alitoa ujumbe maalum wa kumtakia matashi mema Padre Salawa katika Safari yake ya utume wa Upadre, huku akimwelezea kuwa, huduma za kiroho anazozitoa zinawagusa moja kwa moja wananchi wa Jimbo la Itwangi analoliongoza.

Mbunge wa Jimbo la Itwangi Mheshimiwa Azah Hilal Hamad 

Pia alitumia nafasi hiyo kuwakumbusha waaamini waliouhuduria Misa hiyo na wananchi kwa ujumla kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya mvua za El Nino zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini, ikiwemo katika mkoa wa Shinyanga.

Amewasisitiza kuwalinda watoto ili wasipatwe na madhara ikiwemo hatari ya kusombwa na maji.

Padre Salawa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Jimbo Katoliki Shinyanga, alipewa Daraja ya Upadre mnamo Julai, 27, 1995, katika Parokia ya Ng’wandoya Wilayani Meatu mkoani Simiyu, ambayo kwa sasa iko katika Jimbo jipya la Bariadi.

Post a Comment

0 Comments