Uchaguzi huo wa viongozi wa RUJAT, ulifanyika jana tarehe 31, Oktoba, 2026, katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Dodoama, Jijini Dodoma.
![]() |
| Mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi Felix Mwakyembe akitangaza matokeo |
![]() |
| Mwenyekiti wa RUJAT Neville Charles Meena akizungumza baada ya kuchaguliwa kwa mara nyingine kukiongoza chama hicho |
Wakati huohuo, wanachama wa RUJAT wamemchagua Bi. Hamida Ramadhan kutoka mkoa wa Dodoma kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, ambapo Bw. Prosper Laurent Kwigize kutoka Kasulu mkoani Kigoma, amechaguliwa kwa mara nyingine tena kuwa Katibu wa chama hicho kwa kura 76 kati ya kura 77 zilizopigwa.
![]() |
| Bw. Prosper Laurent Kwigize, Katibu wa RUJAT |
Kikao hicho
pia kimemchagua Zena Mohamed Chitwanga kuwa Mweka hazina wa RUJAT.
Wanachama wa
RUJAT pia wamewachagua wajumbe saba wa Kamati tendaji, ambao ni Musa Juma Siwayombe, Devotha Martine Paul,
Malunde Kadama na Rashid Abdullah
Mtagaluka.
Wengine
waliochaguliwa kuwa wajumbe wa Kamati hiyo ni Anna Robi, Andrea Ashery Ngolola
na Fadhili Abdallah Mwangamola.
Kwa mujibu wa mabadiliko ya Katiba yaliyopitishwa na wanachama wa RUJAT, Uongozi wa Meena na wenzake utadumu kwa muda wa miaka minne, kabla ya kufanyika uchaguzi mwingine.





0 Comments