![]() |
| SACP Janeth Magomi (mwenye Miwani) akizungumza na Bodaboda Maganzo |
Leo
Jumatano tarehe 7, Oktoba, 2026, amekutana na kuzungumza na waendesha bodaboda Kanda ya Maganzo
Wilayani Kishapu, ambapo pamoja na mambo mengine amewapatia elimu kuhusu usalama, utii wa
sheria, amani na utatuzi wa changamoto zinazowakabili katika shughuli zao.
Akizungumza na kundi hilo kupitia Mkutano maalum uliofanyika kwenye Uwanja wa Sabasaba katika
mji wa Maganzo, Kamanda Magomi amewataka waendesha bodaboda kulipa kipaumbele
cha kwanza suala la usalama wao na abiria wanaowabeba, pamoja na kuzingatia
sheria zote za usalama barabarani bila kusubiri shurutishwa na Jeshi la Polisi.
Kamanda Magomi ambaye alikuwa ameambatana na maafisa, wakaguzi na Askari wa Polisi wa vyeo mbalimbali, ameisisitiza jamii kwa ujumla wake kuzingatia suala la amani na utulivu, huku akibainisha kuwa, hatua hiyo ndiyo msingi wa wananchi kufanya shughuli za maendeleo na uzalishaji mali, ikiwemo shughuli za usafirishaji zinazofanywa na Bodaboda.
Pia
amewakumbusha wananchi na Bodaboda kushiriki kwa ukamilifu Kampeni ya
Usalimishaji wa Hiari wa Silaha Haramu, inayomalizika Oktoba 31, 2026.
Aidha,
amewataka kuchukua tahadhari zote zinazotakiwa dhidi ya mvua za El Niño
zinazotarajiwa kunyesha msimu huu.
Kupitia Mkutano huo, Kamanda Magomi amechangia Shilingi Laki moja katika mfuko wa waendesha bodaboda hao, huku akiwahamasisha kuimarisha umoja na kuwa na utaratibu wa kusaidiana kwa mambo mbalimbali ya kijamii .
Hata hivyo,
wamewasilisha changamoto ya kutopata leseni za kuendeshea vyombo vya moto,
licha ya baadhi yao kusoma mafunzo na kupata vyeti kutoka vyuo walivyosomea.
Wamesema changamoto hiyo inatokana na baadhi ya vyuo hivyo kutotambulika au
kutokuwa vimesajiliwa katika mfumo.
Akijibu changamoto hiyo, Kamanda Magomi ameahidi kuwasaidia kwa kuwaunganisha na wakufunzi kutoka vyuo vilivyosajiliwa ili wapewe mafunzo kwa gharama nafuu, waweze kupata vyeti vinavyotambulika na hatimaye kukata leseni za udereva.







0 Comments