Zaidi ya abiria 40 wamenusurika kifo, baada ya basi la abiria mali ya Kampuni ya Abood kuteketea kwa moto katika eneo la Isaka, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga.
Tukio hilo
limetokea leo, Novemba 13, 2026, majira ya saa 11 alfajiri.
Basi hilo lenye namba za usajili T 285 EAV, lilikuwa safarini
kutoka Dar es Salaam kuelekea mkoani Kagera.
Akizungumzia
tukio hilo, Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Kahama, ASF Stanley
Luhwago, amesema kikosi cha zimamoto kilipata taarifa na kufika eneo la tukio,
ambapo kilifanikiwa kuudhibiti na kuuzima moto huo.
Kutokana na
tukio hilo, abiria wote waliokuwamo ndani ya basi hilo wamenusurika, huku basi
hilo likiteketea kwa moto.
Chanzo cha moto huo na thamani ya mali iliyoteketea bado havijaelezwa.


0 Comments