Tukio hilo lilitokea Agosti 25, 2026, majira ya saa 1:00
usiku katika Barabara Kuu ya Dar es Salaam–Morogoro.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Salim Morcase, amesema
gari aina ya Toyota Noah lenye namba za usajili T 804 ERM, lililokuwa likitokea
Dar es Salaam kuelekea Mlandizi, liliwagonga askari hao baada ya dereva
kulipita gari lililokuwa limesimama kupisha waenda kwa miguu.
Amesema askari Izdory Michael alifariki papo hapo, huku
askari wa kike, Rehema Magawa, akijeruhiwa na kukimbizwa Hospitali ya Rufaa ya
Tumbi, ambako alifariki dunia asubuhi ya Agosti 26, 2026 kutokana na majeraha
ya kichwa.
Kwa mujibu wa Kamanda Morcase, dereva alikimbia baada ya
ajali, lakini Polisi kwa kushirikiana na wananchi walifanya msako na
kulifanikiwa kulipata gari hilo majira ya saa 2:40 usiku eneo la Kwamfipa,
Wilaya ya Kibaha, lilipokuwa limefichwa.
Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya
Tumbi ikisubiri taratibu za kusafirishwa kwa ajili ya mazishi.

0 Comments