Kauli hiyo
imetolewa leo Bungeni na Naibu Waziri wa Fedha, Laurent Luswetula, wakati
akijibu swali la Mbunge wa Mpanda Mjini, Haidary Sumry, aliyetaka kujua iwapo
Serikali inaweza kupunguza riba za mikopo ya biashara ili kuwawezesha
wafanyabiashara kulipa madeni kwa wakati.
Luswetula
amesema Serikali haiingilii moja kwa moja upangaji wa riba, lakini inaendelea
kuchukua hatua za kisera na kiusimamizi kuwezesha wananchi kupata mikopo kwa
gharama nafuu.
Amesema Serikali pia imeanzisha mfumo wa Price Comparator, unaowawezesha wakopaji kulinganisha viwango vya riba na gharama za mikopo katika taasisi mbalimbali za fedha, hivyo kufanya maamuzi sahihi na kuongeza ushindani unaoweza kuchangia kupunguza gharama za mikopo.

0 Comments