Mkuu wa majeshi ya Uganda, Muhoozi Kainerugaba, ametangaza
kuwa atawania urais katika uchaguzi wa mwaka 2031.
Muhoozi ambaye ni mtoto wa Rais Yoweri Museveni, aliyeitawala Uganda tangu mwaka 1986, ametangaza kuwania nafasi hiyo ya juu zaidi nchini mwaka 2031, na amedai atashinda kwa neema ya Mwenyezi Mungu.
Muhoozi aliandika katika ujumbe mfululizo kwenye mtandao wa X Jumanne usiku.
Mwanajeshi huyo mwenye umri wa miaka 52 pia amesema anaamini kuwa akipata uungwaji mkono wa baba yake, atashinda uchaguzi huo kwa asilimia 90. Kwa muda mrefu amekuwa akitajwa kuwa mrithi anayeandaliwa kuchukua nafasi ya Museveni.
Muhoozi ambaye anaongoza kundi la kisiasa la Patriotic League of Uganda. aliwahi pia kutangaza nia ya kuwania urais katika uchaguzi wa Januari 2026, lakini baadaye alijiondoa na kumuunga mkono baba yake.

SOURCE:DW

0 Comments