Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ametangaza kujiuzulu wadhifa wake kuanzia Septemba 4, 2026, ikiwa imesalia miezi michache atimize mwaka mmoja tangu ashike wadhifa huo pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan.
Katika barua ya Agosti 25, 2026 iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii, Nchimbi amesema amemwandikia Rais Samia kumjulisha kuwa ameamua pia kustaafu siasa na utumishi wa umma.
Nchimbi amesema uamuzi wake umefanywa kwa kuzingatia Ibara ya 50(2)(c), ikisomwa pamoja na Ibara ya 149(2) ya Katiba ya Tanzania. Ibara hizo zinaweka mazingira na utaratibu wa mwenye dhamana ya kikatiba kujiuzulu.

0 Comments