Akizungumza na Shinyanga One Media, Mganga Mfawidhi
wa hospitali hiyo, Dkt. Pierina Mwaluko, amesema maboresho hayo
yanatokana na kuwepo kwa vifaa vya kisasa, vilivyotolewa na Wizara ya Afya,
kupitia mpango wa Serikali wa kuboresha huduma za afya.
Amesema kwa sasa hospitali hiyo ina wataalamu wanne wa tiba mazoezi, ambapo mmoja yuko masomoni kwa ajili ya kuongeza ujuzi.
Ameongeza kuwa, huduma hiyo inatolewa kwa wananchi wote wakiwemo
wagonjwa wa nje na waliolazwa Hospitalini hapo, kwa kuchangia gharama kidogo
kulingana na miongozo iliyotolewa na wizara ya Afya.
Amesema upatikanaji wa huduma hiyo katika hospitali hiyo
umesaidia kupunguza changamoto iliyokuwa ikiwakabili wananchi, ambao awali
walilazimika kwenda katika hospitali binafsi jijini Mwanza au Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kupata huduma hizo.
Kwa upande wake, mtaalamu wa tiba mazoezi katika hospitali
hiyo, Elihuruma Keppa, amesema kwa sasa wanahudumia wagonjwa kati ya 10
na 20 kwa siku wenye mahitaji mbalimbali ya tiba mazoezi.
Amesema wagonjwa wanaofika kupata huduma hiyo ni pamoja waliopooza baadhi ya sehemu za miili kutokana na magonjwa mbalimbali kama kiharusi, waliojeruhiwa katika ajali, watoto wenye changamoto ya mfumo wa fahamu, wenye maumivu ya mgongo, shingo, nyonga na misuli na wenye ulemavu wa viungo,
Wameeleza kuwa upatikanaji wa huduma hiyo karibu na makazi yao umewaondolea usumbufu na gharama za kusafiri umbali mrefu kama ilivyokuwa awali.
0 Comments