RAIS SAMIA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA VIONGOZI WA KANISA KATOLIKI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan, amekutana na kuzungumza na viongozi wa Kanisa Katoliki nchini, kupitia Baraza la maaskofu Katoliki Tanzania TEC.

Rais Samia amekutana na viongozi hao Jumatatu tarehe 10, Agosti, 2026, Ikulu Chamwino Jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa kutoka Ofisi ya Rais, Rais Samia amezungumza na viongozi hao kuhusu masuala mbalimbali ya kitaifa, ikiwemo amani, mshikamano, maendeleo, na umuhimu wa viongozi wa dini katika kujenga jamii yenye maadili na uwajibikaji.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa, Rais Samia amewahakikishia viongozi hao dhamira yake ya kuendelea kushauriana na kushirikisha viongozi wa dini na makundi mbalimbali katika masuala mauhimu yanayojenga mustakabali wa taifa.

Viongozi waliokutana na Rais ni pamoja na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Mhashamu Wolfgang Pisa, OF.M.Cap, ambaye pia ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi, Makamu wa Rais wa TEC Mhashamu Eusebius Nzigilwa, ambaye pia ni Askofu wa Jimbo la Mpanda na Askofu Mkuu wa jimbo kuu la Tabora Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa.

Wengine ni Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Mwanza Mhashamu Renatus Nkwande, Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Arusha Mhashamu Isaac Amani, Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dodoma Mhashamu Beatus Kinyaia na Katibu mkuu wa TEC Padre Dkt.Charles Kitima.

Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Mwanza Mhashamu Renatus Nkwande (katikati) na Katibu mkuu wa TEC Padre Dkt.Charles Kitima (kulia)

Post a Comment

0 Comments