MLIPUKO WA EBOLA DRC WAENDELEA KUSABABISHA VIFO VYA WATU

 

Watu 2,325 wamefariki dunia kutokana na mlipuko wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), huku idadi ya walioambukizwa ikifikia 4,945, kwa mujibu wa takwimu za serikali zilizotolewa Jumapili.

Idadi hiyo ya vifo imevuka vifo 2,299 vilivyoripotiwa katika mlipuko wa mwaka 2018–2020, na kuufanya mlipuko wa sasa kuwa mbaya zaidi kuwahi kutokea nchini humo.

Takwimu hizo zinaonesha pia kuwa visa vipya 101 viligunduliwa ndani ya saa 24 zilizopita, hali inayoendelea kuongeza wasiwasi kuhusu kasi ya kuenea kwa ugonjwa huo.

Mlipuko huo unasababishwa na virusi vya Bundibugyo, aina ya virusi vya Ebola ambayo kwa sasa haina chanjo wala tiba iliyoidhinishwa.

Mamlaka za afya zinaendelea kuimarisha hatua za kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo, huku wataalamu wakisisitiza umuhimu wa kugundua wagonjwa mapema na kuwapatia matibabu kwa wakati.

Source DW

 


Post a Comment

0 Comments