RAIS HICHILEMA AONGOZA KATIKA MATOKEO YA UCHAGUZI ZAMBIA

 

Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema, anaongoza katika matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais, baada ya matokeo kutoka majimbo 135 kati ya 226 kutangazwa.

Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi ya Zambia, Hichilema amepata kura 1,544,140, sawa na asilimia 58.87, huku mpinzani wake mkuu, Brian Mundubile, akipata kura 1,030,662.

Mgombea anapaswa kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura halali ili kushinda katika duru ya kwanza.

Uchaguzi huo ulifanyika kwa kiasi kikubwa kwa amani, ingawa upinzani uliripoti vitisho, ukamataji na matukio ya vurugu.

Zoezi la kuhesabu kura lilisimamishwa kwa takribani saa sita baada ya maafisa wa uchaguzi kushambuliwa na kura kuibwa, kabla ya kuanza tena.

Waangalizi wa kimataifa wamevitaka vyama vya siasa kuepuka kauli za uchochezi na kusubiri matokeo ya mwisho, yanayotarajiwa kutangazwa Jumatatu.

source DW

 

Post a Comment

0 Comments