MWENGE WA UHURU WAPOKELEWA MKOANI SHINYANGA, MIRADI 45 IKIWEMO YA SEKTA BINAFSI KUFIKIWA

 
Jumla ya miradi 45 ya maendeleo, itatembelewa, kukaguliwa , kufunguliwa na kuwekewa mawe ya msingi katika mkoa wa Shinyanga, kupitia mbio za Mwenge wa Uhuru ambazo zimeanza mkoani Shinyanga hii leo.

Akipokea Mwenge huo kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Mwanza Said Mtanda, Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita, amesema miradi itakayofikiwa na Mwenge huo kwa pamoja ina thamani ya Shilingi Bilioni 18, ambapo kati ya hiyo, 13 itawekewa mawe ya msingi, 17 itazinduliwa, 4 itafunguliwa na 11 itatembelewa na kukaguliwa.

Baada ya Mwenge wa Uhuru kupokelewa mkoa wa Shinyanga, leo umeanza mbio zake katika Wilaya ya Kishapu ambapo kati ya miradi iliyozinduliwa ni pamoja na tawi la Benki ya CRDB Maganzo, ambayo itahudumia wananchi wa eneo hilo wakiwemo wachimbaji wa madini ya Almasi, wakulima wa mazao mbalimbali ikiwemo pamba na wafugaji.

Kesho Jumatano tarehe 19, Agosti 2026, Mwenge wa Uhuru utapokelewa na kukimbizwa katika Manispaa ya Shinyanga, ambapo miradi mbalimbali ya maendeleo itatembelewa, kukaguliwa na kuzinduliwa.

Post a Comment

0 Comments