Baba Mtakatifu Leo XIV tarehe, amemteua Askofu mkuu Angelo
Accattino kuwa ni Balozi mpya wa Vatican nchini Colombia.
Kabla ya uteuzi huo, Askofu mkuu Accattino alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini
Tanzania.
Askofu mkuu Accattino ambaye ana shahada ya uzamivu katika
sheria za Kanisa, alizaliwa tarehe 31
Julai 1966 nchini Italia.
Baada ya masomo yake ya Kipadre tarehe 25 Juni 1994 akapewa
Daraja Takatifu ya Upadre.
Alianza utume wake katika masuala ya diplomasia ya Kanisa,
tarehe 1 Julai 1999 ambapo tangu wakati huo, akatekeleza utume wake huko
Trinidad na Tobago, Colombia, Perù, Vatican na hatimaye, Marekani na Uturuki.
Baba Mtakatifu Francisko tarehe 12 Septemba 2017 akamteua
kuwa Balozi wa Vatican nchini Bolivia na kumpandisha hadhi kuwa ni Askofu mkuu
na kuwekwa wakfu kama Askofu mkuu tarehe 25, Novemba 2017.
Tarehe 2 Januari 2023 akateuliwa na Baba Mtakatifu
Francisko kuwa Balozi wa Vatican nchini Tanzania na hatimaye, 15 Agosti 2026
Baba Mtakatifu Leo XIV amemteua kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini
Colombia.

0 Comments