Afisa msimamizi kodi mkuu wa TRA makao makuu Bw. Philipo Eliamini, ameimbia Shinyanga One Media kuwa, hatua hiyo imetokana na mabadiliko ya vipengere mbalimbali vya sheria ya kodi, ambayo yamekuja kufuatia mabadiliko ya sheria ya fedha ya mwaka 2026, yaliyopitishwa na Bunge kupitia bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha 2026/2027.
Amesema
mfanyabiashara mwenye vigezo vilivyobainishwa anatakiwa kuwasilisha mwenyewe maombi
ya kupewa msamaha TRA, na baade atapewa fomu maalum ambayo atajaza taarifa
muhimu za biashara yake, ili aweze kufanyiwa tathmini.
Baada ya
tathmini kufanyika na TRA kujiridhisha na taarifa alizoziweka, atapewa msamaha wa kodi kwa muda wa miezi 12, ambapo baada ya
kipindi hicho kupita, ataendelea na
utaratibu wa kawaida wa kodi.
Hata hivyo, kwa wale ambao mauzo yao yataendelea kuwa chini ya Shilingi Milioni 4 kwa mwaka hata baada ya muda wa miezi 12 kupita, amesema wataendelea na msamaha wa kodi kama Sheria ya kodi inavyoelekeza.
Bw. Eliamini ameeleza kuwa, utekelezaji wa sheria hiyo tayari umeanza kuanzia tarehe 1, Julai, 2026, na ametumia nafasi hiyo kuwahimiza wananchi kufungua na kusajili biashara zao, ili kunufaika na msamaha huo.
0 Comments