TUME YA KUCHUNGUZA WAHUSIKA WA GHASIA ZA UCHAGUZI HAITAINGILIWA NA MAMLAKA YOYOTE

 
Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya Uchunguzi wa Wahusika wa Ghasia na Ukiukwaji wa Sheria katika matukio yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Shaban Ali Lila, amesema Tume hiyo iko huru na haiingiliwi na mamlaka yoyote katika kutekeleza majukumu iliyopewa.

Jaji Lila ametoa kauli hiyo leo Agosti 24, 2026, jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari, akiwataka wananchi kuwa na imani na Tume hiyo.

Amesema kwa mujibu wa Sheria ya Tume za Uchunguzi, mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuunda Tume, huanza kutekeleza majukumu yake kwa utaratibu wa kimahakama kama inavyofanya Mahakama Kuu.

Tume hiyo iliundwa na rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, Mei 18,2026, kutokana na mapendekezo ya tume ya Jaji Mkuu mstaafu Athman Chande, iliyochunguza matukio ya ghasia wakati na baada ya uchaguzi wa oktoba, 2025.

SOURCE: TBC

Post a Comment

0 Comments