Wakizungumza kupitia Redio Faraja ya mjini Shinyanga, Maafisa Sheria wa Tume hiyo, Vick Mbunde na Richard Mdee, wamesema, mtu yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo hivyo anakuwa ametenda kosa la jinai na anaweza kuhukumiwa kifungo cha hadi miaka 20 jela au faini isiyozidi Shilingi milioni 100, au kiasi chenye thamani mara tatu ya mali iliyohusika katika soko kwa wakati huo.
![]() |
| Afisa Sheria wa Tume ya kurekebisha Sheria Tanzania Vick Mbunde |
![]() |
| Afisa Sheria wa Tume ya kurekebisha Sheria Tanzania Richard Mdee |
Makosa
mengine ni pamoja na kushiriki katika njama za kutenda uhalifu huo, kujaribu
kuutekeleza, kusaidia au kuwezesha kufanyika kwake, pamoja na kuficha ukweli au
kuzuia upatikanaji wa taarifa zinazohusiana na vitendo vya utakatishaji wa
fedha.
Wameyataja
madhara ya utakatishaji wa fedha kuwa ni pamoja na kutishia Amani na usalama wa
taifa na jamii, kuchochea vitendo vya
ugaidi kutokana na uwezekano wa fedha hizo kutumika kufadhili shughuli hizo,
kuongeza uhalifu na kuwezesha kuibuka kwa magenge ya kihalifu yanayotumia nguvu
ya kifedha.
Aidha,
wameonya kuwa, vitendo vya utakatishaji wa fedha vinatishia ustawi wa nchi na
kuathiri ukuaji wa uchumi, kwa kuwa fedha zinazotokana na uhalifu huo zinaweza
kutumika kutoa rushwa ili kupata nguvu za kimamlaka kwa ajili ya kuendeleza shughuli
haramu, pamoja na kudhoofisha biashara na shughuli za kibenki.
Maafisa hao
wamebainisha kuwa, sheria inazitaka taasisi
za kifedha, wakaguzi wa fedha, mawakala wa huduma za kifedha, wafanyabiashara
wa magari, wahasibu, madalali, mawakala wa kodi, watoa huduma kwa kampuni,
kampuni za usambazaji na usafirishaji wa bidhaa pamoja na kampuni za bima kutoa
taarifa kwa mamlaka husika ndani ya saa 24, kuhusu miamala inayotiliwa shaka.
Wamezitaja mamlaka zinazopaswa kupewa taarifa kuwa ni kitengo cha kudhibiti biashara ya fedha haramu (FIU) au katika Jeshi la Polisi.




0 Comments