RAIS SAMIA AUNDA TUME YA UCHUNGUZI WA KIJINAI YA GHASIA ZA OKTOBA 29, 2025

Rais wa Jamhauri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua Tume ya Uchunguzi wa Kijinai itakayochunguza kwa kina ghasia zilizotokea wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025, na kubaini waliohusika, waliochochea na waliofadhili matukio hayo.

Akizindua tume hiyo Agosti 7 Ikulu Jijini Dar es salaam, Rais Samia amesema uchunguzi huo unalenga kwenda mbali zaidi ya kazi iliyofanywa na Tume ya Jaji Mohamed Chande Othman, ambayo ilichunguza mazingira na athari za uvunjifu wa amani ulioandamana na uchaguzi huo.

Tume mpya inaongozwa na Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania, Shabani Ally Lila. Mbali na majaji wa Tanzania, imejumuisha pia Naibu Jaji Mkuu wa Namibia Petrus Tileinge Damaseb na Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Uganda Barishaki Cheborion.

Rais Samia amesema kuwajumuisha majaji kutoka nchi hizo mbili kunalenga kuipa tume mtazamo mpana zaidi. Uganda ni mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC, huku Namibia ikiwa mwanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, SADC.

"Tume hii inakwenda kuingia kwa undani zaidi kutafuta nani hasa," Samia amesema, akieleza kuwa uchunguzi unapaswa kubaini waliohusika, waliochochea na waliotoa fedha kwa ajili ya ghasia.

 

Post a Comment

0 Comments